×

Sirro Awanasa Vinara wa Kufoji Kadi za Chanjo Homa ya Manjano!

sirroDAR ES SALAAM: Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba ambao ni vinara wa kutengeneza kadi bandia za chanjo ya homa ya manjano walizokuwa wakiziuza kwa watu mbalimbali katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ili kuwafanya waweze kusafiri nje ya nchi.

Watuhumiwa hao walikuwa wakiuza kadi hizo za bandia kwa watu waliokuwa wakisafiri bila hata ya kupata chanjo hiyo.

sirro-2

Kamishna wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro akionyesha wanahabari baadhi ya kadi hizo walizozikamata.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro, alisema Januari 16, mwaka huu, walipata taarifa za uwepo wa watuhumiwa hao na jeshi la polisi likafika na kufanikiwa kuwatia nguvuni.

“Tulipata taarifa kutoka kwa raia wema ambapo polisi walifika maeneo hayo ya Mnazi Mmoja na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao saba,” alisema Kamanda Sirro huku akiwataja watuhumiwa hao kuwa ni Aisha Juma (29) mkazi wa Vingunguti, Yakobo Wilson (42) mkazi wa Chanika, Oliver Juma (58) mkazi wa Kigogo, Judith Dastani (23) mkazi wa Kiwalani, Fredy Nyomeye (44) mkazi wa Changombe, Salum Nassoro mkazi Chanika Magengeni  na Mohamed Godfrey mkazi  wa Majohe, Gongo la Mboto.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao walipohojiwa, walikiri kutenda kosa hilo la kufoji kadi hizo hivyo upelelezi ukikamilika, watawafikisha mahakamani.

Stori: Denis Mtima/GPL

 

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam