UINGEREZA: STAA wa muvi ya ‘The Elephant Man’, ambaye ameifanya kazi ya uigizaji kwa zaidi ya miongo 6, Sir Joh Hurt amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 77 kwa ugonjwa wa kansa na matatizo ya tumbo.
Kwa miaka mingi, staa huyo ambaye filamu ya kwanza iliyomtoa ilikuwa ni A Man For All Seasons ya mwaka 1966, kwa miaka mingi alikuwa akipambana na ugonjwa wa saratani ambapo hivi karibuni, alilazimika kukatisha kurekodi filamu mpya ya The Entertainer baada ya kushauriwa kufanya hivyo na daktari kutokana na matatizo ya kiafya.
Hurt amedumu na mkewe, Anwen Rees-Myers kwa miaka 12, na miongoni mwa kazi zake za mwishomwisho zilizompa heshima, ni pamoja na filamu ya maisha ya mke wa rais wa zamani wa Marekani, John F. Kennedy iitwayo Jackie alikoigiza kama mchungaji. Filamu hiyo imeingia kwenye orodha ya kuwania Tuzo za Oscar mwaka huu.
Baadhi ya muvi maarufu alizocheza katika tasnia hiyo kwa zaidi ya miaka 50 kuanzia mwaka 1962 ni;
1962 The Wild and the Willing
1966 A Man For All Seasons
1978 The Midnight Express
1978 The Lord of the Rings
1979 Alien
1980 The Elephant Man
1984 Nineteen Eighty-Four
1989 Scandal
1991 King Ralph
1998 Night Train
2001 Captain Corelli’s Mandolin
2001 Harry Potter and the Philosopher’s Stone
2002 Miranda
2002 Crime And Punishment
2003 Dogville
2004 Hellboy
2004 Pride
2005 Valiant
2006 V For Vendetta
2008 Indiana Jones and the Kingdom of the Crystal Skull
2009 New York, I Love You
2009 44 Inch Chest
2010 Brighton Rock
2010 Harry Potter and the Deathly Hallows – Part 1
2011 Harry Potter and the Deathly Hallows – Part 2
2011 Melancholia
2011 Tinker Tailor Soldier Spy
2014 Hercules
2016 Jackie
2017 That Good Night
2017 My Name Is Lenny
