
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa-Tanzania, John Shibuda Magalle, akizungumza na wanahabari.
MWENYEKITI wa Baraza la Vyama Vya Siasa-Tanzania, John Shibuda Magalle, ametoa wito kwa Watanzania kumuunga mkono Rais John Magufuli katika utendaji kazi wake katika jamii.
Shibuda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wahabari jjiini Dar es Salaam alipompongeza Rais Magufuli na Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, na viongozi wote wa serikali ya awamu ya tano kwa juhudi zao katika kuwaletea wananchi maendeleo. 
Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza, akifafanua jambo.

Baadhi ya wanahabari na viongozi kutoka Baraza la Vyama Vya Siasa waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Aidha amevitakia vyama vya siasa mafaniko mema katika utendaji kazi zao hususani vinapouanza mwaka mpya wa 2017. Pia aliwatakia mafanikio viongozi wote wadhamini wa makundi mbalimbali ya utumishi kwa kutekeleza kikamilifu kazi za ustawi wa jamii na wa taifa letu.
Kwa taarifa kamili tembelea www.globaltvtz.com ili kupata kikamilifu alichozungumza Shibuda.
NA DENIS MTIMA/GPL