×

Beki anayeongoza kwa mabao

laurent-koscielny-420413

MAKALA | CHAMPIONI | LONDON, England

UNAPOTAJA mas­taa katika Premier huwezi kulisikia jina la Laurent Koscielny likita­jwa, lakini huyu ni mmoja wa mabeki bora katika ligi hiyo.

Pengine jina lake halitajwi kwa sababu anacheza katika nafasi ya ulinzi na kasumba ya soka ni kwamba ni vigu­mu kwa mabeki kutajwa, unapozungumzia mas­taa. Mara nyingi huta­jwa zaidi watu wanao­funga mabao.

Koscielny, 31, wiki iliyo­pita alifikisha mechi ya 200 akiichezea Arsenal kwenye Ligi Kuu England, hakuna anayejua hilo au hata kama wanajua, basi wameamua kunyamaza.

Rekodi zake katika mechi hizo 200 za Premier ni balaa. Mfaransa huyu amejiimari­sha katika safu ya ulinzi ya Arsenal na hivi sasa anach­eza kwa kuelewana vilivyo na ingizo jipya, Shkodran Mus­tafi.

Tangu atue Arse­nal akitokea ka­tika kikosi cha Lo­rient ya Ufaran­sa, beki huyu ame­kuwa nguzo muhimu katika kikosi cha The Gunners na hata akiko­sekana dimbani kwa sababu yoyote ile, pengo lake limekuwa ni vigu­mu kuzibika.

Wiki iliyopi­ta, mkali h u y u asiyetajwa sana, alifikisha mechi yake ya 200 kwenye Premier akiwa na Ar­senal huku kwa ujumla akiwa amecheza mechi 274 za michuano yote na kufunga mabao 22. Kwenye Premier amefunga mabao 17.

Laurent KoscielnyLakini usisahau kuwa katika mch­ezo wake wa 200 wa Premier akiwa na Arsenal iliy­okuwa ikiivaa Burnl e y , ndiye aliyesababisha penalti ya dakika ya 97, iliyotumiwa vyema na fowadi Alexis Sanchez kuipatia Arsenal bao la ushindi na kuondoka uwanjani kifua mbe­le ikiwa imeshinda 2-1. Hiyo ilikuwa ni baada ya Burnley kusawazisha katika dakika ya 93.

Koscielny huy­uhuyu ndiye aliye­funga bao la utata la mkono katika mch­ezo wa kwanza wa Arsenal na Burnley dakika za mwisho na kuifanya timu hiyo iondoke uwanjani na pointi tatu muhimu baada ya kushinda 1-0.

Koscielny, aliye­muoa mwan­a m k e mrem­bo Claire Beaudouin na ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mpya, ana rekodi kibao alizo­tengeneza tangu atue Arsenal na ny­ingi huenda hazifa­hamiki kwa kuwa hasikiki kiaina.

laurentkoscielnyarsenalvmonacoykpjhty0y9zl

 

REKODI:

Koscielny ni Mfaran­sa wa nne kufikisha mechi 200 za Pre­mier akiichezea Ar­senal na ni mchezaji wa 15 kwa ujumla kufikisha mechi 200 za Premier ka­tika historia ya klabu hiyo.

Kwa kipindi cha misimu saba tan­gu atue Arsenal, hakuna mchezaji mwingine wa Arse­nal aliyecheza mechi nyingi kama Kosciel­ny. Ndiye aliyeitumi­kia timu hiyo mara nyingi zaidi kuliko mwingine yeyote tangu wakati huo.

Koscielny pia ameshinda ‘tackling’ nyingi zaidi hadi sasa msimu huu k u l i k o wakat i m w i n g i n e wowote katika msimu uliopita. Hadi sasa ‘ame-tack­le’ mara 30.

laurent_koscielnyUsisahau kwamba Koscielny ndiye aliyefunga mabao mengi zaidi ya Pre­mier kuliko beki mwingine yeyote katika historia ya Arsenal. Amefunga mabao 17.

Mechi ya kwanza ya Koscielny katika Premier akiwa na uzi wa Arsenal ili­kuwa ni Agosti 15, 2010 dhidi ya Liver­pool kwenye Uwan­ja wa Anfield, mche­zo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 na alitolewa uwanjani kwa kadi nyekundu dakika za mwisho­ni.

Koscielny hadi sasa amecheza wastani wa dakika 84 kwa mechi kwani ametolewa uwanja­ni kama ‘sub’ mara 13 tu tangu alipo­tua Emirates.

WACHEZAJI  WA ARSENAL WALIOFIKISHA MECHI ZA PREMIER 200 NA ZAIDI:

David Seaman 325

D.Bergkamp 315

Martin Keown 310

Lee Dixon 305

Patrick Vieira 279

Nigel Winterburn 270

Thierry Henry 258

Tony Adams 255

Theo Walcott 252

Kolo Toure 225

Freddie Ljungberg 216

Bacary Sagna 213

Cesc Fabregas 212

Laurent Koscielny 200

TAKWIMU ZA

KOSCIELNY:

Dakika alizocheza: 16,813

Mechi ambazo hajaruhusu bao: 76

Mabao: 17

Asisti: 2

Tackles alizoshinda: 261

Kushinda mipira ya juu: 62%

Kazuia mipira: 580

Kagusa mpira mara: 11,666

Kaokoa hatari mara: 1,204

Kasababisha faulo: 170

Njano: 26

Nyekundu: 4.