×

Droo ya Kwanza Mbagala Zakheem

DROO NDOGO YA SHINDA NYUMBA (6)

Mshiriki wa Droo ya Shinda Nyumba akiandaliwa kuokota  Kuponi.

SASA Global Publishers imeweka wazi kuwa droo ya kwanza kati ya nyingi ndogondogo kwa ajili ya shindano lake la Shinda Nyumba Awamu ya Pili, itachezeshwa katika viwanja vya Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam Februari 8, mwaka huu.

DROO NDOGO YA SHINDA NYUMBA (1)

Kuponi za Shinda Nyumba zikiwekwa pamoja ili zoezi la kuokota lianze.

 Ikumbukwe kuwa droo hiyo ndiyo itakuwa kifungua njia kuelekea kumpata mshindi wa nyumba ya mamilioni ya shilingi, kwenye droo itakayochezeshwa mwishoni mwa bahati nasibu, baada ya kuwa zimeshafanyika ndogondogo kadhaa katika maeneo mbalimbali.

shinda-nyumba-7

Mr Championi (kulia) akigawa zawadi ya Tisheti kwa mmoja wa washiriki wa Shinda Nyumba.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema jana kuwa baada ya jana Mr Championi kugawa zawadi kwa wasomaji waliokutwa wakijaza kuponi za shindano hilo, anatumia nafasi hiyo kuwatangazia wasomaji na washiriki kuwa droo ndogondogo sasa zitachezwa kila mwezi.

 “Ni rasmi sasa kuwa kutakuwa na droo ndogo kila mwezi kuanzia sasa hadi siku ya droo kubwa, katika droo hizo zawadi mbalimbali zitatolewa zikiwemo pikipiki, televisheni, vyombo vya ndani na simu za kisasa,” alisema Mrisho.

10.Wakazi wa eneo la Mkoa wa Pwani-Kibaha wakiweka kuponi zao ndani ya ndoo maalum ili kushiriki droo ya puili ya Shinda Nyumba.

Afisa Masoko Jimmy Haroun (Mwenye Kofia)  akiwaelekeza washiriki namna ya kuwekaa kuponi zao.

Katika kuona jinsi gani wasomaji wamelipokea shindano hilo la awamu ya pili, timu ya Shinda Nyumba ya Global Publishers wiki iliyopita ilizunguka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na wasomaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa na Championi. Wengi wa wasomaji hao katika mitaa ya Msasani, Tandale, Magomeni, Mwananyamala, Sinza, Goba, Tegeta, Madale, Kigogo na kwingineko ambako wamejitokeza kwa wingi kununua magazeti na kujaza kuponi kwa ajili ya kushinda nyumba awamu ya pili, walielezea shauku yao ya kuona safari hii nao wanaibuka kuwa washindi.

8.Wasoamaji wa Gazeti la Ijumaa na Championi wakiweka kuponi zao ili kushiriki droo ya pili ya Shinda Nyumba.-001

 

 “Nawakubali sana Global na mimi nimeamua kushiriki baada ya kugundua kuwa Shinda Nyumba ni ya ukweli baada ya kumuona mshindi toka mkoani Iringa akizungumza mwenyewe kuwa kashinda kwa kununua magazeti yenu,” alisema  Yusuph wa Tandale.

Wakazi wa Goba ambao pia walitembelewa na timu ya Shinda Nyumba, nao walisema hawawezi kukaa kimya bila kupata kuponi za shindano hilo wakati kila mmoja hivi sasa anazungumzia kuhusu zawadi bwerere kutoka Global Publishers.

shinda-nyumba-11

Baadhi ya washiriki wa Shinda Nyumba wakijaza kuponi

 “Siyo lazima mtu ushinde nyumba maana hiyo ni zali la mentali kweli, lakini jamani hivi vitu kama simu na vyombo vya nyumbani uvikose? Mimi natamani sana simu ya tachi, nitajaza kuponi hadi nipate,” alisema Consolata Simon, aliyekutwa kijiweni kwake kwa mama ntilie, huko Goba.

14.Mafundi Gereji wa Kibaha nao wakionekana kuchangamkia kununua gazeti ili kuweza kushirki droo ya pili ya Shinda Nyumba.

Mshiriki (kulia)akinunua Gazeti.

 Msomaji mwingine Unaris Yunus, wa Goba njia panda, alisema awamu ya kwanza ya Shinda Nyumba hakuweza kupata zawadi yoyote, lakini safari hii moyo wake unamsukuma kuamini atakuwa miongoni mwa washindi. “Kwanza nasikia zawadi zimeongezeka, sasa kama mnavyosema pikipiki itatolewa kila mwezi, sasa nikose nyumba sawa, basi pikipiki, televisheni, simu, mashuka, blanketi hadi vyombo vya ndani nikose, aaah jamani, Mungu nisaidie,” alisema Yunus.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho alizidi kuwasisitiza wasomaji kuhakikisha wanajipatia kuponi za kutosha tayari kwa droo ndogo ya kwanza ambayo itafanyika hiyo Februari 8, mwaka huu.  “Utaratibu wetu wa kutuma kuponi ni uleule, baada ya kununua gazeti letu lolote kati ya Championi, Risasi, Uwazi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda, kata kuponi kisha jaza kwa kadiri ilivyoelekezwa, halafu peleka kwa wakala yeyote aliye jirani na wewe, maana mawakala wetu wapo nchi nzima, au kwa wale wa Dar es Salaam, wanaweza kuzileta katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar,” alisema.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam