×

Wenger: Mnatamani kuniona gerezani siyo

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kuwa watu wengi wanatamani sana leo angekuwa amefungwa gerezani.

Wenger amefungiwa kukaa kwenye benchi la timu yake kwa mechi nne na hadi sasa ameshatumika mbili, lakini anasema wale wanaosema kuwa adhabu hiyo ni ndogo walikuwa wanatamani kumuona amefungwa gerezani.

Kocha huyo amefungiwa michezo hiyo baada ya kumsukuma mwamuzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Burnley wiki moja na nusu iliyopita.

“Wengi wasionitaka watazidi kuona kuwa adhabu hii ni ndogo sana.

“Wanatamani kuniona nimewekwa gerezani sehemu fulani, nafi kiri hapo ndiyo watakuwa na furaha sana.”

Wenger tayari ameshatumika kwenye michezo miwili, dhidi ya Southampton na mchezo wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Watford. Sasa ataendelea kukosa michezo mingine miwili dhidi ya Chelsea Jumamosi na dhidi ya Hull.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam