×

Yaliyojili Kwenye Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Sheria Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017

Rais Magufuli akizungumza na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamisi Juma  wakati wa uzinduzi huo.

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma akihutubia wakati wa uzinduzi huo.

Rais Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi huo.

Rais Magufuli akipokea ripoti ya mahakama kuhusu kesi za uchaguzi kutoka kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma.

Rais Magufuli akikabidhi kwa Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  ripoti ya mahakama kuhusu kesi za uchaguzi wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama.

Rais Magufuli akiagana na majaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama Kuu baada ya sherehe za uzinduzi huo.

Rais Magufuli akiaga baada ya sherehe hizo.

Rais Magufuli akipeana mikono na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu  baada ya sherehe hizo.
DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo Februari 2017, amezindua Mwaka Mpya wa Kimahakama wakati wa sherehe zilizofanyika katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amezipongeza mahakama zote kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiwaahidi kutatua kero zinazowakabili ikiwemo miashahara midogo.
Aidha Rais Magufuli amewataka majaji na mahakimu wote nchini kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania wenzao.
Machache aliyozungumza rais Magufuli yakoi hapa.

SIKU_YA_SHERIA: Nashukuru kwa kuona kazi nzuri zinazofanywa na mahakama hapa nchini –

SIKU_YA_SHERIA: Endapo mahakama, wapelelezi na polisi na mawakili nyote mkifanya kazi hivi Tanzania itakuwa na amani sana –

SIKU_YA_SHERIA: Mwaka jana mahakimu 28 walishtakiwa kwa makosa mbalimbali mengine yakiwemo ya rushwa lakini wote walishinda – 1/3

SIKU_YA _SHERIA: Hii inaweza kuleta picha mbaya, labda upelelezi haukufanyika vizuri, mahakimu waliosimamia kesi hizo walibebana-2/3

SIKU_YA _SHERIA: Watu wazuri wasichafuliwe na wachache, naomba muwasafishe kabisa – 3/3

SIKU_YA _SHERIA: Hizo ni baadi tu ya changamoto kwenye sekta ya mahakam ni kwamba watumishi wke ni wachache ukilinganisha na sekta nyingine.

SIKU_YA _SHERIA: Kwa nini kuwe na walinzi wa mahakama 1900 wa nini? Kwa nini msitumie polisi na makampuni ya ulinzi? –

SIKU_YA _SHERIA: Naibu Jaji Mkuu, nikuhakishie kwamba nafasi ambazo kweli zinahitaji kuongezewa watumishi nitalifanyia kazi – 1/2

SIKU_YA _SHERIA: Lakini bafasi ambazo sio za lazima fanyeni mbinu zingine –

SIKU_YA _SHERIA: Nchi hii wakwepa kodi ni wengi, na wanaheshimiwa, kiasi cha Sh. Trilioni 7.5 hazijakusanywa 1/3

SIKU_YA _SHERIA: Yawezekana tatizo ni la TRA lakini niwaombe watu wa mahakama mtusaidie. – 2/2

SIKU_YA _SHERIA: Niwaombe majaji mtende haki ili kufanikisha hilo –

SIKU_YA _SHERIA: Kati ya majaji 80 waliosafiri nje mwaka jana, 6 pekee walilipiwa na serikali, 74 walijilipia wenyewe –

SIKU_YA _SHERIA: Nani ambaye hafahamu kwamba ofisi za DPP na AG zinagombana zenyewe kwa zenyewe na wapo ofisi moja? – 1/2

SIKU_YA _SHERIA: Niwaombe DPP na AG kwa kushirikiana na waziri, tafuteni njia ya kutatua hayo matatizo –

SIKU_YA _SHERIA: Mtu anakamata na meno ya tembo au madawa ya kulevya, haitakiwi kesi kuahirishwa ahukumiwe hapo hapo? 1/3

SIKU_YA _SHERIA:Anayekuja kumtetea aunganishwe huko huko, awekwe ndani ili akija kuomba rufaa awe ameshaonja joto la jiwe. 2/3

SIKU_YA _SHERIA: Kama umemkamata na meno ya tembo unaahirisha eti upelelezi haujakamilika unataka mpaka ukamate na nini. 3/3

Save

Save