
Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani akizungumza na waandishi wa Global Publishers alipotembelea ofisi za Global.
Kailima akitoa elimu ya mpiga kura.
Ofisa wa Tume ya Uchaguzi, akikagua jina la mpiga kura Salum Milongo kwenye, zoezi lililofanyika kwenye ofisi za Global Publishers, kutoka kulia ni Mhariri wa Gazetio la Uwazi, Elvan Stambuli, Mhariri wa Ijumaa Wikienda, Sifael Paul, mwandishi wa Championi, Khadija Mngwai pamoja na mtangazaji wa Global TV, Kelvin Shayo.
Mwandishi wa Habarai, Musa Mateja ‘mpiga kura’ akipiga kura za majaribio kwenye chumba maalum cha kupigia kura.
Musa Mateja baada ya kupiga kura.
Zoezi likaendelea.
‘Mawakala wa wagombea’ wakiwa kwenye zoezi hilo.
Mwandishi Omary Mdose ‘akipiga kura’
Mwandishi, Wilbert Molandi ‘akipiga kura’

Maofisa wa tume ‘wakihesabu kura’.
Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (wa pili kushoto) akimshukuru Kailima kwa ujio wake Global Publishers 
Kailima akimwaga kura zote kwa ajili ya kuhesabiwa.


Maofisa wa NEC wakiingiza taarifa za matokeo kwenye mfumo wa Kompyuta
Kailima akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani na wafanyakazi wa taasisi hiyo kwa mara ya kwanza Tanzania wameanza kutoa elimu ya mpiga kura kwa wafanyakazi wa Global Publishers leo.
Zoezi hilo lilifanyika katika ofisi za Global Publishers, Bamaga Mwenge jijini Dar ambapo Kailima alitumia muda mwingi kujibu maswali ya waandishi wa habari na wafanyakazi wengine na baadaye akaonesha ‘laivu’ jinsi ya zoezi la upigaji wa kura unavyofanywa mpaka hatua ya kutangazwa matokeo na kutangaza kwamba zoezi hilo litafanyika nchi nzima.
“Nimeamua kuja hapa, hiki ni chombo cha habari cha kwanza Tanzania kuwaonesha zoezi hili. Kwa jinsi mlivyoona hapa, ni vigumu sana mgombea kuiba kura, naamini nyinyi mtakuwa wajumbe kwa kufikisha kwa wananchi haya tuliyoonesha hapa,” alisema Kailima.
Alifafanua kuwa elimu ya mpiga kura itakuwa ikitolewa na tume yake ya uchaguzi nchi nzima ili wapiga kura wajue haki yao na jinsi ya kuhakikisha kwamba kura za wagombea wao zinakuwa salama kwa kuwa na mawakala kila hatua ya upigaji kura mpaka wakati wa kuhesabu na kutangazwa mshindi.