×

Moto waunguza Genge la Mama Lishe, Nyumba ya Mama JB yanusurika kuungua Sinza

Gari la zima moto likifika eneo la tukio na kukuta moto huo umekwishazimwa na wananchi.

MCHANA wa leo, moto umeunguza genge la mama lishe aliyejulikana kwa jina la Mama Wambura lililopo Sinza Mori na kunusurika kuungua nyumba iliyodaiwa kuwa ya mama mzazi wa mwigizaji wa Bongo Muvi, Jacob Steven ’JB’ iliyokuwa jirani na genge hilo jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya vijana wakichota maji kwa ajili ya kuzimia moto huo.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamesema kuwa chanzo cha moto huo hakikufahamika mara moja kwani mmiliki wa genge hilo hakuwepo wakati moto huo unawaka.

“Mwenye genge hili huwa anafika asubuhi anaandaa chakula na inapofika nyakati za mchana huanza kuwasambazia wateja wake katika maduka yao, huenda aliacha majiko ya gesi yakiwaka ndio ikawa chanzo cha moto huu,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Baadhi ya wananchi wakidhibiti moto huo kwa kuuzima na maji.

 

 

NA DENIS MTIMA/GPL