
DAR ES SALAAM: Raha nyingine ya ubuyu ni kuupata ule ambao ni orijino! Staa wa kitambo wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Mtangazaji wa Radio Times FM ya jijini Dar, Yvonne Cheryl Ngatikwa ‘Monalisa’ au ‘Mona’, amekwaa skendo matata ya mwanaye aliyejifungua hivi karibuni kudaiwa kuwa na baba watatu na ndiyo sababu ya kutopenda kumuanika.

Kama hiyo haitoshi, wamwaga ubuyu pia wanadai kwamba, eti mtoto huyo ni mweupe ‘pee’ hivyo wengine kwenda mbali zaidi na kushusha madai mazito kuwa, huenda baba yake ni Mwarabu au Mchina.

Kama kawaida, Wikienda huwa halilazi damu hivyo linakupa ubuyu kutoka kwa wambeya mtaani ambao waliufikisha mezani na kuomba Mona abanwe sababu ya kutoonesha sura ya mtoto wake huyo kama alivyokuwa akiinadi mimba yake mitandaoni kabla ya kujifungua.

MSIKIE MTOA UBUYU:
“Jamani kama mtakumbuka Mona aliunadi sana ujauzito wake mitandaoni tangu ukiwa mchanga lakini baada ya kupata mtoto, amekuwa kimya haposti mitandaoni.

“Unaambiwa hata watu wanaoruhusiwa kwenda kumuona mtoto ni wachache, tena kwa masharti ya kutopiga naye picha, huoni kama kuna kitu hapo?
“Inasemekana Mona kuna kitu anaficha maana wanatajwa ‘wababa’ watatu (majina yanahifadhiwa), ingawa ukimwangalia mtoto wake ni mweupe sana huenda akawa Mwarabu.
“Lakini huu ni ubuyu tu, ngoja mtoto akue ndiyo ukweli wote tutaujua,” alisema sosi.
AFANYA 40 KUBWA, AMBANIA MTOTO
Ubuyu uliendelea kunyetishwa kwamba, baada ya mwanaye kutimiza siku arobaini (40), hivi karibuni Mona alifanya sherehe kubwa ambayo ilijumuisha mastaa kibao, lakini pia haikuonekana sehemu ambayo alimuonesha mtoto wake huyo. Ilisemeka kwamba, katika shughuli hiyo, hata picha zilizotupiwa mitandaoni zilikuwa ni zile za mashosti zake tu bila za mtoto mwenyewe aliyekuwa anafanyiwa shughuli yake.

MONA ABANWA, AFUNGUKA
Baada ya ubuyu huo kujaa tele kwenye meza ya Wikienda, Mona alitafutwa na alipopatikana alifunguka kwa ghadhabu akidai kuwa hapendi kumwanika mwanaye huyo kwa sababu si mtoto wa mtu na kwamba ni uzao wake hivyo ni uamuzi wake kumwanika au asimwanike.

Mahojiano kati ya Wikienda na Mona yalikuwa kama ifuatavyo;
Wikienda: Mona mambo vipi? Mbona hutaki tuje kukupa hongera? Hata hivyo, ubuyu unadai kuwa tangu ujifungue hutaki kuonana na waandishi kwa ajili ya mahojiano unaficha nini?
Mona: Nihojiwe ili iweje? Je, habari zangu za kujifungua zinasaidia nini jamii?
Wikienda: Wewe ni staa, watu wana hamu ya kujua kama wanavyofuatilia mastaa wengine na kujifungua ni jambo jema, kwa nini unaficha hivyo?
Mona: Kimya.
Wikienda: Inasemekana kuwa hutaki watu wakuone na mwanao unamficha…
Mona: Jamani namficha kwa sababu ni mtoto wangu kwani kuna tatizo gani jamani?
Wikienda: Inasemekana kuwa mwanao ana baba watatu, wengine wanasema ni Mwarabu, je, unalizungumziaje hilo?
Mona : Dah! Nini wat
atu? Acha waseme hata kama ana baba kumi.
NENO LA MHARIRI Kwanza tunampa Mona hongera kwa kujifungua, Mungu ampe makuzi mema mtoto wake. Mambo ya kuhusu baba anajua Mona mwenyewe lakini pia kuonesha mtoto si jambo baya na kwa kuwa ni staa hata mwanaye anaingia kwenye orodha ya mastaa ndiyo maana mashabiki wake wana shauku ya kumuona