Kesi ya Lissu na Wenzake, Shahidi wa Jamhuri Atoa Ushahidi - Global Publishers
Imewekwa na on February 14th, 2017 , 08:43:53pm

Kesi ya Lissu na Wenzake, Shahidi wa Jamhuri Atoa Ushahidi

DAR ES SALAAM: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo imeanza kusikiliza ushahidi wa upande wa jamhuri juu ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa watatu, Mhariri wa Gazeti la Mawio, Simon Mkina, Jabir Idrisa, Tundu Lissu na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.

Watuhumiwa hao, wanadaiwa kwamba, kwa kipindi cha kuanzia Januari 12 hadi 14, 2016 katika Jiji la Dar es Salaam, kwa pamoja waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko Yaja Zanzibar’ kwenye Gazeti la Mwanahalisi.

Shahidi wa kwanza upande wa jamhuri alikuwa ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani ambaye alitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma