×

Diva: Siwezi Kudate na Mwanamme Ambaye Hajui Kuzungumza Kiingereza

KAMA ulikiuwa hujui kamata hii nakutonya! Endapo ulishawahi kufikiria kumnyapia mtangazaji wa Kipindi cha Ala za Roho, Diva The Bause, hakikisha Kiingereza chako kimenyooka wala siyo cha ‘you, me and the’.

Diva ameanika sifa namba moja ya mwanamme ambaye hupendezwa kudate naye ni yule amabaye anafahamu kuzungumza lugha ya Kiingereza kwa ufasaha. Kama hajui Kiingereza Diva hashughuliki naye kabisa!

Akifanya Exclusive Interview nqa Global TV Online, wakati wa hafla ya Valentines iliyoandaliwa na mwigizaji Irene Uwoya pale Next Door usiku wa kuamkia leo.

Alipoulizwa kuhusu aina ya wanaume anaowapenda hasa kwenye swala la mahaba, Diva alijibu hivi…

“Napenda kudate na mwanamme anayefahamu kuzungumza Kiingereza, kama hajui basi siweji hata kujaribu kudate naye…” Alisema Diva.

Full interview nimekuwekea hapa, pitia pitia Global TV Online ucheki stori zote kali.