
DAVIDS Bwana mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Feza amefanikiwa kuibuka mshindi wa pili barani Afrika wa kuandika insha juu ya mambo ya utaalamu wa anga, tuzo ambazo zinazoandaliwa na Multi Choice Afrika kwa kushirikiana na Shirika la Anga la Eutelsat.

Shindano hilo lilifanyika Februari 7, Lagos, Nigeria ambapo washindi walitangazwa baada ya kamati inayohusika na mashindano hayo kukutana mjini humo chini ya mwanamama Claudie Haignere.




Tuzo za Dstv Eutelsat Star Awards 2017 niza mara ya sita kufanyika zikishirikisha takribani shule 1,000 kutoka nchi 20 barani Afrika na miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Tanzania , Nigeria Ethiopia na Botswana.