Namna ya Kuishi na Maadui wa mpenzi wako
Imewekwa na on February 16th, 2017 , 01:05:44pm

Namna ya Kuishi na Maadui wa mpenzi wako

Na ASHA BARAKA| GAZETI LA AMANI| SINDANO LA MASTAA

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu? Bila shaka Valentine ilikwenda vizuri kwako na unaendelea vyema na maisha yako ya uhusiano. Mpenzi msomaji wangu leo utakuwa nami Asha Baraka, Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta katika kolamu hii ya Sindano za Mahaba na bila kukupotezea muda naomba niende kwenye mada moja kwa moja.

Mada niliyokuandalia hapa inahusu namna ya kukabiliana na changamoto ikiwa marafiki, ndugu au watu wa karibu hawaivi chungu kimoja na mpenzi wako.

Naomba nianze kwa kusema wazi kuwa, unapochagua mpenzi si rahisi kumridhisha kila mtu wako wa karibu, yaani wote wakavutiwa naye au kufurahia tabia zake, ni jambo gumu mno kutokea.

Hata ukioa au kuolewa na mtu mwenye mvuto wa kuvutia kwa kiwango cha Wema Sepetu au mwenye tabia nzuri kupindukia bado wapo watakaomchukia. Ninamaanisha katika dunia hii unapofanya jambo usitegemee kumfurahisha kila mmoja.

Mara kwa mara wataalamu wa masuala ya mapenzi wamekuwa wakisema zungumza na moyo wako kwanza unapohitaji kuwa katika uhusiano na mtu fulani. Ndiyo, ninayasema haya nikifahamu kuwa ni muhimu zaidi unapojenga ‘nyumba yako’ kuzingatia vipi huyo uliyenaye ataishi na ndugu zako au watu wako wa karibu.

Sasa inapotokea unaona hakuna uhusiano mzuri kati ya pande hizi mbili, jambo la kwanza kabisa unalotakiwa kufanya ni kuzisikiliza pande zote mbili. Msikilize mpenzi wako akupe sababu ya tofauti hizo na wasikilize watu wako wa karibu. Katika hili hutakiwi kuonyesha upendeleo upande wowote ule, jitahidi kuweka mazingira sawa ukiwaahidi wote kulifanyia kazi tatizo lililopo.

Lakini inapotokea ukaona kuna mazingira ya ‘kuwachana’ ukweli  watu wako wa karibu unapoona sababu zao hazina mashiko, fanya hivyo ili wauelewe wazi msimamo wako uko wapi. Hata hivyo, katika hali nyingine ya kukabiliana nao, jiepushe wewe na mpenzi wako kutupiana nao maneno au kuwasema pembeni. Puuzia kila kitu na suala la muhimu kuwa bize na familia yako. Itafika wakati watakuelewa tu kuwa uko ‘serious’ na huyo uliye naye.

Hivyo tu basi! Kuna watu wengi sana wamewapoteza wapenzi wao na watu wao waliowapenda maishani mwao na kupanga nao mambo mengi kutokana na namna watu wao wa karibu wanavyowaangalia hao wapenzi wao au kuwachukulia.

Haipaswi kuwa hivyo, ni lazima mtu kuwa na msimamo wa ndani kabisa unapokuwa katika hili hutakiwi kuonyesha upendeleo upande wowote ule, jitahidi kuweka mazingira sawa ukiwaahidi wote kulifanyia kazi tatizo lililopo. Lakini inapotokea ukaona kuna mazingira ya ‘kuwachana’ ukweli watu wako wa karibu unapoona sababu zao hazina mashiko, fanya hivyo ili umedhamiria kujenga familia yako mwenyewe.

Nifahamu hapa mtakuwa mmenielewa. Akili ya kuambiwa changanya na yako mpenzi msomaji wa kolamu hii na usifikirie kama nilivyosema hapo mwanzo kuwa itatokea siku umridhishe kila mtu katika uchaguzi wako. Nikutakie kila la kheri katika kujenga uhusiano na mpenzi wako ili kuandaa maisha ya baadaye pamoja na familia yenu

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma