Wanawake na Tatizo la Vinyweleo Usoni
Imewekwa na on February 16th, 2017 , 10:02:20am

Wanawake na Tatizo la Vinyweleo Usoni

Na WAANDISHI WETU| GAZETI LA AMANI| TIPS ZA UREMBO

MAGANDA ya machungwa, malimao huondoa vinyweleo usoni WANAWAKE wengi hulala-mikia tatizo la kutokwa na vinyweleo vingi kwenye miili yao. Wengine hutumia mbinu ya kuvinyoa kwa kutumia wembe ambapo badala ya kuvipunguza, husababisha viongezeke na ngozi za nyuso zao kuzeeka. Badala ya kutumia krimu kali au wembe, maganda ya limao au maganda ya machungwa, yanaweza kukusaidia kuondoa vinyweleo hivyo.

MAHITAJI

-Unga wa maganda ya machungwa au malimao kijiko kimoja. Unaweza kuandaa unga huo kwa kuyakausha maganda hayo juani kwa siku kadhaa kisha ukayatwanga na kuyasaga kupata ungaunga wake.

-Vijiko viwili vya mafuta ya mzaituni (olive oil)

-Kijiko kimoja cha unga wa mtama

-Kijiko kimoja cha maji ya waridi (rose water).

NAMNA YA KUANDAA

-Changanya unga wa maganda ya machungwa au malimao na unga wa mtama kwenye chombo kimoja kisha ongeza mafuta ya mzaituni pamoja na maji ya waridi. Changanya mpaka upate ujiuji mzito.

-Jipake ujiuji huo usoni na uache ukae kwa dakika kumi. Baada ya hapo, tumia vidole vyako vya mikono kuisugua ngozi yako kwa namna ya kutengeneza mduara, zoezi hilo lidumu kwa dakika tano hadi kumi kisha baada ya hapo, osha uso wako kwa maji safi. Fanya zoezi hilo kila siku kwa kipindi cha wiki mbili hadi tatu, utaona mabadiliko.

Tupia Comment Yako, Matusi Hapana

Stori zinazo husiana na ulizosoma