×

#BongoCelebrityNews: Feza Kessy; Sihitaji Mwanaume Tajiri, Mshamba wa Mademu… (+VIDEO)

USIKU wa kuamkia Feb 18, 2017 wa Bata Batani kwenye uzinduzi wa Video ya SHUGA ya Mimi Mars  pale Masaki, Club Next Door. Global TV Online inafanikiwa kumnasa mtangazaji wa Choice FM, Feza Kessy na kumfanyia Interview ili kufahamu mambo machache kuhusu yeye na kasha sisi kukusogezea wewe upate kuyaelewa maisha ya staa huyo toka kitambo.

Swali la kwanza kwa Feza Ilikuwa ni kutaka kujua endapo ana mpenzi na kama hana ni kwa nini?===> “Hamuwezi kumjua shemeji, maana Wabongo nawafafamu, ukimuanika tu halafu siku mkija kukosana watakuongea mpaka basi kwa hiyo mimi namficha na mapenzi yangu ni ya siri.

Vipi kuhusu vigezo vya mwanamme wa kudate naye? ===>“Mwanamme nayeweza kumpenda kutoka naye ni yule ambaye kwanza havai skin jeans (suruali za jeansa za kubana mwili), napenda avae timberland, tsheti huyo napendezwa naye lakini asiwe mwanamme wa chips mayai (akimaanisha legelege).

Feza Kessy naquick Rocka.

Kuhusu mtonyo kwa mme atakayemuoa? ===>“Atakayenioa siyo lazima awe na pesa nyingi, kwanza nataka aniheshimu pili asiwe mshamba wa mademu, maana mimi mwenyewe nina wivu hatari. Kama amekuja kwangu atulie sizani kama bado unaendelea kuzunguka. Hela yake itutoshe tu sio lazima awe tajili wa kupindukia.

Kuhusu wivu wa mapenzi je? ===>“Mimi nina wivu sana, kama natoka na mwanamme lazima nikague simu yake, niingie inbox na email nasoma pia lakini hata yeye namruhusu kukagua simua yangu.” Alimalizia Feza.

MTAZAME FEZA KESSY AKIANIKA KUWELI WAKE HAPA