×

Muller The Machine! Mbaya wa Arsenal Anayetakiwa Man United

Na WAANDISHI WETU| CHAMPIONI JUMAMOSI| MICHEZO NA BURUDANI

IKIWA na miaka 16 kwenye kikosi cha Bayern Munich, Thomas Muller ni miongoni mwa washambuliaji hodari na ghari duniani na haishangazi kusikia Manchester United ikimtaka.

Jumatano usiku alikuwa mwiba mchungu kwa Arsenal alipofunga bao la tano dakika ya 88 ikiwa ni sekunde 120 baada ya kuingia dakik a ya 86 na kuiwezesha timu yake ya Bayern Munich kushinda mabao 5-1. Kabla ya mchezo huo kulikuwepo na habari za Man United inayofundishwa na Jose Mourinho kumuhitaji Muller kwenye kikosi chao tena wakaweka mezani dau la pauni milioni 85 sawa na Sh bilioni 232.

Mourinho baada ya kuwasajili Eric Bailly, Zlatan Ibrahimovic, Henrikh Mkhitaryan na Paul Pogba kwa zaidi ya pauni milioni 145 (zaidi ya Sh bilioni 395.8) msimu huu, sasa anamtaka Muller ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.

OFA YA MAN UNITED YAKATALIWA

Makamu Mwenyekiti wa Bayern Munich, Jan-Christian Dreesen klabu yake imepiga chini ofa ya Man United ya kutaka kumsajili Muller kwa ofa ya pauni milioni 85 ikisema bado inamuhitaji kikosini. Dreesen anayeshughulika zaidi na mambo ya fedha ya klabu hiyo, amethibitisha kushindwa kwa Mourinho katika mpango wake huo wa kumsajili Muller kwenda England kwa mara nyingine.

Thomas Muller

Alipotakiwa kuthibitisha kama alipokea ofa ya pauni milioni 85 kutoka Man United, Dreesen anasema:”Kuna kitu kama hicho, ikaja fax kutoka England. Kwetu sisi hatujawahi kuzungumza k u h u s u mauzo ya Thomas Muller, hatujazungumza lolote kumhusu yeye. ”

Kama mchezaji anatusaidia, tutakuwa wapuuzi tukimpa mkataba wa muda mfupi kutegemea na faida tutakayopata kutoka kwake.” Inaonekana Man United sasa imeanza harakati za kumtaka Muller kwa nguvu baada ya kuonekana kuna ugumu wa kumpata Antonio Griezmann wa Atletico Madrid kwani tayari kuna vikwazo kadhaa.

THOM AS MULLER

Muller ni raia wa Ujerumani na alizaliwa Septemba 13, 1989 huko Weilheim, Oberbayern, Ujerumani Magharibi. Sasa ana urefu wa futi 6 na inchi 1, kikosini anamudu kucheza nafasi za straika, winga na kiungo mshambuliaji wa kati. Muller alicheza katika akademi ya TSV Pahl mwaka 1993 hadi 2000 alipojiunga na akademi ya Bayern Munich.

Mwaka 2008 hadi 2009 alikuwa anacheza kikosi cha pili cha Bayern hapo alicheza mechi 35 na kufunga mabao 16 na wakati huohuo alikuwa akiitwa kucheza kikosi cha wakubwa. Tangu 2008 hadi leo, Muller ameichezea Bayern mechi 245 na kufunga mabao 92. Tangu mwaka 2004, ame-chezea timu za taifa za watoto za Ujerumani kuanzia chini ya miaka 16, 19, 20 na 21. Anachezea kikosi cha wakubwa cha Uje2009 alikuwa anacheza kikosi cha pili cha Bayern hapo alicheza mechi chezea Bayern mechi 245 na kufunga mabao 92.

Tangu mwaka 2004, ame-chezea timu za cha wakubwa cha Uje245 na kufunga mabao 92. Tangu mwaka 2004, rumani kuanzia mwaka 2010 hadi leo akiwa amecheza mechi 83 na kufunga mabao 36. Muller katika fainali za Kombe la Dunia 2010, alifunga mabao matano na kuiwezesha Ujerumani kushika nafasi ya tatu na kuwa mfungaji bora akiwa na mabao hayo matano na asisti tatu.

Mwaka 2014 huko Brazil, Muller aliisaidia Ujerumani kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia na yeye kuwa mfungaji namba mbili akiwa na mabao matano na kuchaguliwa katika kikosi bora cha Kombe la Dunia. Hata hivyo katika Ligi Kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’ msimu huu, Muller amefunga bao moja tu katika mechi 17 alizocheza huku akifunga matano katika mechi za michuano yote.

AIFANYA KITU MBAYA ARSENAL

Jumatano usiku wiki hii, Muller akiichezea Bayern dhidi ya Arsenal katika mchezo wa 16 Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Allianz Arena, dakika ya 88 alifunga bao la tano na kuiwezesha timu yake kushinda mabao 5-1. Mabao mengine ya Bayern yalifungwa na   Arjen Robben dakika ya 11, Robert Lewandowski dakika ya 53, Thiago Thiago Alcantara do Nascimento aliyefunga mawili dakika ya 56 na 63. Timu hizo zitarudiana Machi 7, mwaka huu kwenye Uwanja wa Emirates jijini London