×

Yanga Sc Isidharau Kumlipa Ernie Brandts

Na BODI YA UHARIRI| CHAMPIONI JUMAMOSI| MICHEZO NA BURUDANI

HIVI karibuni Yanga ililetewa taarifa ya kutakiwa kumlipa aliyekuwa kocha wake Ernie Brandts malimbikizo ya madai yake ambayo hakulipwa huko nyuma. Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ndilo lililofikia uamuzi wa kuitaka Yanga imlipe Brandts haki zake na kama isipofanya hivyo katika muda uliopangwa inaweza kupokwa pointi zake.

Yanga haitakiwi kuwa na maneno mengi katika utekelezaji wa agizo hili la Fifa kwani huko si kama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
linavyoichukulia timu hiyo, kanuni zinatumika ipasavyo.

Iwe siri au kwa kuweka wazi, Yanga inapaswa kumlipa Brandts ili kuepuka adhabu ya Fifa ambayo inaweza kuiathiri kwa kiasi kikubwa sana katika harakati zake za kutetea ubigwa wa Ligi Kuu Bara.

Ernie Brandts

Mzaha au dharau yoyote ya Yanga katika suala hili unaweza kuigharimu timu hiyo ambayo sasa ipo katika wakati mgumu ndani na nje ya uwanja.