×

EFM Redio Yaacha Historia Mpya Temeke

Jukwaa la mchizi wangu mwaka 2017 lililoleta historia

 

Ilikua ni furaha na shangwe kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam katika msimu huu wa wapendanao ambapo Efm redio ilirudisha shukrani zake kwa wasikilizaji wake hususani wakazi wa Temeke.

 

Umati wa wananchi waliohudhuria tamasha hilo

Efm redio ilitoa shukrani hizo kwa kuandaa tamasha lililotoa burudani ya muziki bure, siku ya Jumamosi ya tarehe 18/02/2017 katika viwanja vya Mwembeyanga na kurushwa moja kwa moja kupitia 93.7 redio efm na kwa mara ya kwanza kupitia kituo cha televisheni cha TV-E.

Sehemu ya mashabiki wa muziki wa singeli wakifurahia baadhi ya burudani zilizokua zikiendelea katika tamasha hilo

Tamasha hilo lilitumbuizwa na wanamuziki wa singeli akiwemo Msaga Sumu, Dogo nigga, Dula Makabila na wengineo wengi na kwamara ya kwanza kwa matamsha ya red.

 

Mwanamuziki wa muziki wa singeli Virus (Mdudu) akitumbuiza jukwaani

 

 

Vilevile Efm redio iliwawezesha madereva bodaboda na bajaji wa wilaya ya Temeke kwa kuwajazia mafuta bure katika vyombo vyao kwa siku sita, kila dereva ambaye chombo chake kina stika ya Efm redio alilazimika kuja na mchizi wake mmoja ambae hana stika hiyo na wote walijaziwa mafuta buree.