×

Usaili wa Shindano la Wikienda Music Search Waanza

Wasanii wakiwa na Emmanuel Ng`osha (aliyevaa miwani) muendeshaji wa mashindano hayo

WASANII wa muziki wa Bongo Fleva mbalimbali Leo wamejitokeza katika usaili wa Shindano la Wikienda Music Search (WMS), uliofanyika katika Studio Zamora Black zilizopo Magomeni Kagera jijini Dar.

Wasanii kibao kutoka viunga vya Jiji la Dar ikiwemo Kigamboni, Kiluvya, Kiwalani, Kimara, Mbezi, Malamba, Chanika, Manzese, Kibamba na wengine kutoka Mkoa wa Pwani.

Ambapo wasanii baadhi watapata kuingia katika mzunguko wa pili wa shindano Hilo. Mshindi atakayeibuka atapata nafasi ya kurekodiwa audio na video ya wimbo wake.  

Emmanuel Ng`osha/GPL