
KAMANDA Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga ameweka wazi sababu zilizofanya staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kutokamatwa barabarani kama wengine wakiwemo vijana wa Singida waliokamatwa kwa kosa la kuendesha gari wakicheza wimbo wa ‘Muziki’ wa Darassa huku dereva akiwa ameachia usukani.

Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani, Kamishna Msaidizi Mohamed Mpinga.
Akizungumza mchana huu katika mahojiano yalioruka Live kupitia Global TV Online, Kamanda Mpinga haya.
Kuhusu vijana wa Singida waliokuwa wakicheza wimbo wa Darassa:
“Kwanza watu wanatakiwa kutambua wale vijana walifanya kosa kubwa la kuhatarisha maisha ambapo dereva aliacha usukani na kuinuka kucheza wimbo. Pili gari likiwa kwenye mwendokasi dereva aliondoka akaenda nyuma huku akisaidiwa na mtu mwingine aliyeshikilia usukani kwa mkono mmoja jambo ambalo lingehatarisha maisha yao.
Kingine wale vijana hawakufunga mikanda jambo ambalo lingehatarisha maisha yao endapo ajali ingetokea wakati huo. Jambo la mwisho kwa wale vijana ni kwamba hawakujisalimisha polisi hadi vijana wetu wapowaweke mtego na kuwanasa hadi wanashikiliwa na kesi inaendelea.“
Kuhusu Diamond Platinumz Je?
“Diamond kosa lake kubwa hakuwa amefunga mkanda na kuna wakati alikuwa akiachia usukani lakini utaona ni tofauti na wale vijana tuliowakamata. Kuachia usukani kwa sekunde kadhaa si kosa na ndiyo maana utaona hata kwenye matengenezo ya magari huwa kwenye kujaribu mtu anaachia kwa muda kuangalia kama gari litapoteza uelekeo.

Diamond alivyokuwa akicheza huku ameachia usukani.
“Kwa hiyo tuliona Diamond ni kioo cha jamii na kitu alichokifanya ni kutofunga mkanda jambo ambalo ni kosa kisheria. Nilimuita akaja ofisini na kujutia kosa.“

Kamanda Mpinga na Diamond Platinumz
Kamanda Mpinga pia alitolea ufafanuzi sababu ya kupiga picha na Diamond angali alitambulika kama mtenda kosa.
“Baada ya kuchukua hatua ya kumuadhibu kwa kosa lake hilo, aliniomba kupiga naye picha na sikuona kama ni jambo baya kumkubalia mtu kupiga naye picha baada ya kujutia adhabu na kulipa faini.”

Kamanda Mpinga (katikati ) akiwa na Viongozi wa Kampuni ya Global Publishers.
Kamanda Mpinga amezungumza mengi juu ya makosa mengi yanayofanywa barabarani na kutolea ufafanuzi mambo kama kwa nini Tanzania tunaendesha spidi mwisho 60, Trafiki kusaidiana na TRA kukamata barabarani, kutolewa matairi bodaboda zinazokatisha kwenye barabara za mwendokasi, viongozi wengi wa siasi kutotia sheria na mengine mengi.
Ili kupata full interview, jiunge nasi kwa kutembelea YouTube Channel ya Global TV Online bila kusahau ku-subscribe.
Credit: Andrew Carlos/GPL
MTAZAME KAMANDA MPINGA AKIZUNGUMZA