
Mwigizaji wa Bongo Movies, Wema Sepetu leo alienda tena katika Mahakama ya Hkimu mkazi Kisutu jijini Dar ambapo kesi yake inaendelea.
Wema aliachiwa kwa dhamana kwenye sakata la dawa za kulevya baada ya kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Staa huyo alifika mahakani hapo huku akionekana mwenye furaha muda wote. Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi 15 March 2017 baada ya upande wa Mashtaka kusema upelelezi bado haujakamilika.