×

Wasanii Bongo Waungana Kuwahamasisha Wanafunzi Msimbazi

Wasanii wa muziki nchini, leo wameungana kwa pamoja kuwapa hamasa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbazi jijini Dar es Salaam kutokana na baadhi ya shule za mkoa huo kushika nafasi za mwisho kwenye matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2016/2017.

Akizungumza wakati wa hamasa hiyo, malkia wa taarab nchini, Khadija Kopa amewaeleza wanafunzi hao kuwa waachane na mambo ya mitandao ya kijamii na badala yake wajikite katika masomo ili waweze kufaulu na kutimiza ndoto zao.

Baadhi ya wasanii waliokuwepo kwenye hamasa hiyo ni pamoja Khadija Kopa, Shilole, Madee, Zimwi Mtu, Sholo Mwamba, Dogo Janja, Gigy Money, Bonge la Nyau, Zushani, Kadjanito na wengine.

Zimwi Mtu akifanya yake.

Bonge la Nyau akiwahamasisha wanafunzi hao.

Msanii wa Singeli, Sholo Mwamba akitoa neno kwa wanafunzi hao.

Khadija Kopa akiwafunda wanafunzi hao.

Bonge la Nyau na Gigy Money.

Msanii Zushani akizungumza.

Wasanii hao wakitoa hamasa.

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS