
NA IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI | MPAKA HOME
NIAJE mtu wangu wa dhahabu? Mimi na wewe sehemu yetu ya kujiachia ni hapa kwa sababu unapata nafasi ya kuweza kuyajua maisha halisi ya mastaa wetu wa fani mbalimbali hapa Bongo wanapokuwa nyumbani.

Leo niko maeneo ya Kijitonyama, nyumbani kwa Video Queen ambaye kwa sasa hivi ana jina kubwa baada ya kuonekana kwenye wimbo wa Nuh Mziwanda unaoitwa Jike Shupa, namzungumzia Zena Abdalah ‘Jike Shupa’ ambaye anaishi nyumbani hapo na mpenzi wake ambaye hakupenda kuamuanika kwa sasa.

Nini anapenda kufanya kama mwanamke akiwa nyumbani?
“Yani mtu yeyote akibahatika kuja kwangu hawezi kukosa kitu cha kula kabisa kwa sababu muda mwingi sana mimi napenda nikiwa nyumbani kama mwanamke nipikepike vitu mbalimbali ndio kazi kubwa napenda kuifanya sana ninapokuwa kwangu.

Maisha yake ya kistaa hayampi kero mchumba wake?
“Hapana hata mara moja na kama nisingekuwa staa kama hivi angenijulia wapi asingenifahamu yeye yuko poa kabisa ana anafurahia ninachokifanya kila wakati.

Kucha zake ni ndefu anafanyaje sasa kazi za nyumbani, kama kufua na vitu vingine?
“Hizi kucha ndio hasa zinanipa mizuka ya kufanya kazi nyingi za nyumbani hazinizuii chochote kabisa maana nguo za mpenzi wangu agusi mtu hata kama nisafiri zinanisubiria mpaka narudi hilo linajulikana na kucha zikiwa hivihivi.

Vipi ana watoto?
“Ndio lakini sipendagi kabisa kuzungumzia hao watu kwa sababu sipendi kuwaweka kwenye vyombo vya habari ila ninao (wangapi amezaa na nani?).


Kitu gani hakipendi?
“Mimi kwa kweli sipendi kabisa umbea kwa sababu mimi ni mtu ambaye napenda sana kuishi na amani sana katika maisha yangu sasa chokochoko na watu sipendagi kabisa





Kitu gani hakipendi?
“Mimi kwa kweli sipendi kabisa umbea kwa sababu mimi ni mtu ambaye napenda sana kuishi na amani sana katika maisha yangu sasa chokochoko na watu sipendagi kabisa.


Naona nyumbani kwako kuna gitaa, unajua kupiga au limekaa kama fasheni?
“Najua kidogo. Naendelea kujifunza zaidi naamini nitakuwa mpigaji mzuri wa gitaa, ngoja nikuonyeshe kidogo namna ambavyo nimeanza kuiva (akaanza kupiga).






Naona mezani kwako kuna pombe kali, ni mpenzi sana wa hivi vitu?
“Hahaha! Siku mojamoja si mbaya najilipua kimtindo lakini zaidi nimewekea wageni ambao wanapenda kutumia maana nyumbani unategemea wageni mbalimbali.
Anazungumziaje ushoga wake na Wema? Ulianza lini?
“Kwanza najua wazi mimi kuwa na ushoga na Wema, watu wanakereka sana lakini ukweli ni kwamba ndio shoga yangu wa damu na nina mpenda niko tayari kununua ugomvi kwa bei rahisi kabisa kwa ajili ya Wema ndio hivyo.”