×

EFM Kusepa na Kijiji Sasa Mikoa Tisa Katika Masafa Yake

EFM radio kituo namba moja kwenye ubunifu na utangazaji mwaka 2016 chenye masafa ya 93.7 kwa miko ya Dar es Salaam na pwani ambacho hujikita katika utoaji burudani, elimu na mafunzo Kwa jamii.

“Katika kuhakikisha Radio inaendelea kutimiza malengo yake iliyojiwekea, imeamua kuongeza masafa yake na kusikika nchi nzima, masafa yatakayoanza kupatikana hivi karibuni katika mikoa tisa ambayo ni Mwanza, Mbeya, Mtwara, Tanga, Babati, Singida, Tabora, Kigoma na Moshi”, alisema Meneja Mkuu wa Efm radio, Dennis Ssebo na kuongeza.

Nikwa miaka mitatu Sasa radio hii imeendelea kuendeaha vipindi vyake,matamasha na Matukio mbalimbali katika mikoa miwili ambayo ni Dar essalaam na pwani.

Awali wananchi ambao matangazo yetu hayakufika walikuwa wakitufuatilia kupitia njia ya mtandao pamoja na mitandao ya kijamii, lakini kwa sasa itakuwa rahisi kwao kusikiliza radio Kwa kupitia masafa husika kwani sio wananchi wrote wenye uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii.

Hivyo kufuatia uongezwaji huo wa masafa ya redi yetu, tunawaomba wasikilizaji na wapenzi wote wanaosikiliza Efm kuendelea kufuatilia zaidi matangazo yetu na kutupatia ushirikiano katika matukio mbalimbali tutakayoyafanya katika mikoa hiyo, alisema.

KATIKA TUKIO HILO, GLOBAL TV ONLINE ILIKUWA LIVE.. BOFYA PLAY UCHEKI HAPA