×

Dodoma: Mmiliki wa Shule Akutwa Uchi, Ameuawa, Akatwa Nyeti

 

Mkurugenzi wa Shule za Zam Zam jijini Dodoma nchini Tanzania, Sheikh Rashid Bura amekutwa amefariki dunia ofisini kwake eneo la Majani ya Chai karibu na Nyerere square jijini humo.

 

Bura ambaye pia Mkurugenzi wa Taasisi ya Islamic Foundation, aliondoka nyumbani kwake zaidi ya siku nne zilizopita na hakujulikani alipokwenda ambapo juhudi za kumtafuta zilifanyika bila mafanikio hadi jana Jumatano Desemba 25, 2019 alipokutwa ofisi kwake akiwa amekufa huku mlango wa ofisi ukiwa umefungwa. 

 

Imedaiwa kuwa mwili wa Bura ulikutwa ukiwa uchi wa mnyama huku akiwa na majeraha ya kisu tumboni na amekatwa uume wake lakini wameuacha unaninginia na huku akiwa amefungwa kamba kwenye kiti.

 

Kanzu yake imekutwa imewekwa pembeni ikiwa haina hata doa la damu. Ikumbukwe mwaka huu maeneo ya Morena Hotel pia mfanyakazi wa TAMISEMI naye alikutwa ameuawa ndani ya gari eneo la Parking.

 

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu alikiri kuwapo kwa kifo hicho lakini akasema wasemaji ni Jeshi la Polisi huku akisema katika imani ya dini ya Kiislamu kifo kinaweza kumkuta mwanadamu mahali popote.

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo lakini alikuwapo wakati mwili huo unachukuliwa jana Jumatano saa moja jioni ukapelekwa mochwari ya Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

 

Wananchi wameomba sasa ulinzi uimarishwe na kamera zifungwe majengo yote muhimu jijini Dodoma. Msiba uko nyumbani kwake Mtaa wa Chang’ombe jijini Dodoma.

 

 

Leave a Comment