×

Makonda Ashiriki Maadhimisho Wiki ya Maji Boko Dar

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Boko ambapo imefanyika maadhimisho ya wiki ya maji akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Baadhi ya vijana wakichota maji katika matenki maalum ya maji yanayotoka DAWASCO.
Meneja wa DAWASCO (kulia mwenye tai) akibadilishana mradi wa maji na mmoja wa wadau wa maji.
Viongozi hao wakiendelea na kuwekeana sahihi ya mradi.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo Machi 17, 2017 ameshiriki katika wiki ya majisafi na Majitaka iliyofanyika Boko, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, ambapo wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali na kutatuliwa kero zao.

Katika kuadhimisha wiki hiyo, pia Makonda ameshuhudia viongozi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) wakitoa elimu, kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi kupitia Dawati Maalumu lililokuwepo eneo hilo.

Hiyo ililenga kutoa mwanya kwa wananchi wanaopata huduma ya maji kutoka Dawasco, kupata Elimu ya Huduma ya Maji na kusikilizwa kero na malalamiko yao ili kujenga ukaribu zaidi kati ya DAWASCO na wananchi.

Pamoja na mambo mengine Dawasco limepokea miradi ya watumiaji maji katika maeneo hayo ya Boko. Maadhimisho ya wiki ya Maji yamebeba kauli mbiu ni Punguza matumizi ya majisafi na rejesha majitaka.