
Wanafunzi watano katika kaunti za #Nakuru, Samburu na Nyandarua wamelazimika kufanyia mitihani yao ya Darasa la Nane (KCPE), Hospitalini baada ya kujifungua Watoto hapo jana (Jumatatu).
Mmoja wa watahiniwa hao (15) kutoka Shule ya Msingi ya Kuresoi, iliyopo Kaunti Ndogo ya Kuresoi Kaskazini, alikimbizwa Hospitalini baada ya kuanza kulalamikia maumivu wakati akiwa Shuleni.
Katika Kaunti ya Nyandarua, Watahiniwa 18 walipata mimba wakati Wanafunzi wakiwa majumbani kutokana na janga la virusi vya Corona hivyo Watahiniwa 11 wanafanya mtihani huo wakiwa Wajawazito.
Aidha, Katika kaunti hiyo hiyo, mtahiniwa (17) kutoka eneo la Njoro anafanyia mtihani wake akiwa mikononi mwa Polisi kwa tuhuma za kumdhalilisha kimapenzi Mtoto wiki moja iliyopita.