
Waziri Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ameunda kamati Maalum ya kuchunguza kitendo kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda cha kuvamia Ofisi za Clouds Media Group, kwa lengo la kushinikiza habari yake irushwe katika kipindi cha De’ Weekend Chat Show (Shilawadu).

Waziri Nape (kulia) akizungumza na wanahabari mapema leo alipotembelea ofisi za Clouds Media, pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media, Joseph Kusaga. Aliyeketi kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), Mzee Reginald Mengi.
Nape ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uaandaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba kuthibitisha kuwa Makonda alivamia kituo hicho, Ujumaa usiku akiwa na polisi wenye silaha.





Mwenyekiti wa MOAT, Mwee Reginald Mengi akiwasili Clouds Media.
“Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi


Huu ni mwendelezo wa sakata la mkuu wa mkoa, kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds FM.
TAZAMA VIDEO HAPA