×

Airtel yazindua ‘HATUPIMI Bando’

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda akizungumza na wanahabari katika hafla hiyo.
Meza kuu ilivyoonekana.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano (katikati) akizungumza katika hafla hiyo.
Beatrice akitoa ufafanuzi wa jambo.
Mabalozi wa ofa ya HATUPIMI ya Airtel, kutoka Kundi la Weusi (Niki wa Pili anayezungumza katikati).

Na Denis Mtima/GPL

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania, leo imezindua ofa kabambe ijulikanayo kama ‘HATUPIMI Bando’ itakayowawezesha wateja wake wote nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.

Airtel HATUPIMI Bando itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisizo na kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi.

Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda alisema: “Tunaleta huduma hizi nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kuwapatia thamani ya pesa zao katika huduma na bidhaa zetu .

“HATUPIMI Bando itawapatia wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau mbalimbali kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali kumalizika kabla ya wakati.

“Kuna vifurushi vya HATUPIMI kwa siku vya hadi Sh 1000 pia vipo vya wiki kwa Sh 5000 na vilevile unaweza kujiunga na HATUPIMI kwa mwezi kwa Sh 10,000, ili ufurahie huduma ya kutopimiwa dakika zako na uongee bila kikomo.

“Airtel tunaamini ofa hii ni ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja wetu na wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe inayowapa uhuru wa kuongea watakavyo bila kikomo.”

Nchunda alifafanua kuwa ili kujiunga na ofa ya HATUPIMI Bando, mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# kisha kuchagua 1 kupata HATUPIMI kisha chagua bando ya siku, wiki au mwezi kulingana na mahitaji yako .

Kampuni hiyo imekuja na ofa hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzindua ofa kabambe kupitia huduma yake ya Airtel Money, vilevile wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua maduka yake 2,000 yatakayotoa huduma kwa wateja ili kuwafikishia huduma popote walipo.