
Jeshi la Israel limekiri kwamba kulikuwa na udhaifu katika kuzuia shambulio la wapiganaji wa Hamas la Oktoba 7, 2024, na kueleza kwamba kwa miaka mingi Israel ilikuwa ikidharau nguvu za wapiganaji hao.
Katika tukio hilo, Hamas waliwaua Waisraeli 1,139 na kuwachukua mateka 200, tukio lililosababisha mapigano makali kati ya Israel na Palestina kuibuka upya na kusababisha maafa makubwa.
Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa jana, Alhamisi, imeeleza kwamba ripoti ya uchunguzi kuhusu tukio hilo imeonesha kuwa Jeshi la Israel (IDF) lilishindwa kuwalinda raia wa Israel.
“Tukio la Oktoba 7 limeonesha kwamba tulifeli, IDF ilifeli kutimiza majukumu yake ya kuwalinda Waisraeli. Watu wengi sana walikufa siku hiyo wakiwa wanajiuliza, ‘IDF wako wapi?'” alikaririwa afisa mmoja wa jeshi la Israel wakati akiichambua ripoti hiyo.