×

Polepole Azungumzia na Vyombo vya Habari, Atangaza Makatibu wa Mikoa, Wilaya

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepople, amesema uhusiano wa chake chake na vyombo vya habari ni wa kihistoria ambapo amesema chama chake kinauheshimu na kitaendelea kuuheshimu uhuru huo.

Polepole aliyesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari na kuzungumza nao masuala mbalimbali yanayoendelea nchini ambapo miongoni mwa mambo mengine alisema kwamba masuala yanayohusiana na viongozi wa chama au serikali, wenye wajibu wa kuyashughulikia ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano, John Magufuli, ambaye ndiye mteuzi wao na pia kwamba masuala mengine yanayohusiana na viongozi kwa upande wa chama, hushughulikiwa kufuatana na taratibu zilizopo.

Iwapo kuna mabadiliko yoyote katika chama chake kuhusiana na mchakato wa kupata mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2020, katibu huyo alisema hakuna kilichobadilika hadi sasa.

Katika hafla hiyo, Polepole alisema kwamba makatibu wakuu wa mikoa wa CCM walioteuliwa ni 31 ambapo 20 miongoni mwao ni wapya ambapo makatibu wa wilaya ni walioteuliwa 76 miongoni mwao ni wapya.

Baadhi ya makatibu hao ni:

MAKATIBU WILAYA CCM

Rehema Ndele- Mbozi

Shaibu Mtawa- Morogoro Vijijini

Alfred Mwambeleko- Masasi

Said Mkoa- Sengerema

Miriam Kaaya- Moshi Vijijini

Agness Msuya- Siha

Mayasa Ayoub- Kilwa

Rafael Maumba- Liwale

Othman Dunga- Hanang

Nuru Ngeleja- Chato

Clemence Mponzi- Kilolo

Mohamed Mfaume- Bukoba Mjini

Mwajuma Boha- Misenyi

Hanafi Msabaha- Kinondoni

Robert Kelenge- Kigamboni

Martin Mwakitabu- Chamwino

Asia Mohameh- Chemba

Ramadhan Dalo- Arusha

Solomoni Itunda- Karatu

Simba Gadafi- Longido

Amos SHimba- Ngorongoro

 

MAKATIBU MIKOA CCM

Amina Imbo- Ruvuma

Haula Kachambwa- Shinyanga

Donald Magesa- Simiyu

Janeth Kayanda- Tabora

Allan Kingazi- Tanga

Kulwa Omary- Morogoro

Zakaria Mwansasu- Mtwara

Raymond Mwangala- Mwanza

Hosea Mpatike- Njombe

Anastazia Amasi- Pwani

Kajolo Peter- Katavi

Naomi Kapambala- Kigoma

Jonathan Marko- Kilimanjaro

Mwanamasoud Pazi- Lindi

Paza Mwamlima- Manyara

Kulwa Omary- Morogoro

Elias Mpanda- Arusha

Jamila Yusuf- Dodoma

Adam Ngalawa- Geita

Christopher- Iringa

Rahel Degeleke- Kagera