
JESHI la Colombia limesema idadi ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi nchini humo imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400. Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana.

Vikosi vya waokoaji vimesema barabara nyingi sehemu kulipotekea maporomoko hayo kusini mwa taifa hilo, Mocoa, hazipitiki kutokana na mkasa huo.

Maporomoko hayo yametokea baada ya mvua kubwa kunyesha kwa saa nyingi.
Aidha viongozi wa mataifa jirani wa Mexico na Argentina walikuwa wa kwanza kutoa ujumbe wa pole na kuahidi kwenda kuisaidia Colombia.