
Baadhi ya wananchi waliofika viwanjani hapo wakishuhudia mashindano hayo.

Baadhi ya washiriki wa shindano la Shika Ndinga wakichuana katika mashindano ya awali ya shindano hilo.

Taswira ilivyoonekana viwanjani hapo.

Hekaheka ikiendelea ya kushika ndinga.

Washiriki kwa upande wa wanawake wakikimbia huku wakishikilia chupa za maji kwenye mashindano ya awali ya Shika Ndinga.

Washiriki wa shindano la Shika Ndinga wakiwa tayari katika mchuano wa kushika ndinga.

Mashindano ya kukimbia na maji kwa utangulizi wa Shika Ndinga kwa upande wa wanaume.

Baadhi ya washiriki wa Shika Ndinga wakiwa wamepumzika kabala ya kuendelea.
Kwa mara nyingine tena Kituo cha Redio cha Efm kimetua Viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam kulinadi Shindano la Shika Ndinga baada ya wiki iliyopita kuzinduliwa rasmi katika Wilaya ya Kigamboni, Dar ambapo litashirikisha wilaya sita za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani
Akirudia tena wito wake kwa wasikilizaji wa kituo hicho cha Efm, meneja mkuu wa kituo hicho, Dennis Ssebo amesema:
“Tunatoa pikipiki 12 katika wilaya sita, tulishatoa pikipiki mbili kwa Wilaya ya Kigamboni na leo tena pikipiki mbili zimechukuliwa na wakazi wawili kutoka wilaya hii ya Temeke, kwa sasa zimebaki wilaya nne za Ilala, Kinondoni, Bagamoyo na Kibaha ambapo mwisho wa mashindano tutatoa magari mawili aina ya Suzuki Cary.”
Pikipiki mbili zinazotolewa kwa kila wilaya, moja huchukuliwa na mwanamke anayeweza kushikilia ndinga (gari) hadi mwisho kwa kuzingatia vigezo vilivyopo na pikipiki nyingine inakwenda kwa mwanaume anayeshinda mtihani wa kushikilia ndinga kulingana na masharti yaliyopo.
“Niseme tu kwamba lengo letu kubwa ni kusaidia jamii kujikwamua kiuchumi kutokana na shindano letu hili linalowawezesha wasikilizaji wetu kupata mtaji kupitia zawadi tunazotoa kwani ni zawadi ambazo watatumia kama biashara za kuwaingizia kipato,” alisema Ssebo.
Katika Wilya ya Temeke, washindi walioibuka kidedea kwa kujinyakulia pikipiki mbili baada ya kushika ndinga hadi mwisho wakiwabwaga wengine, ni Pili Hassan na Abdallah Twaha ambapo wote walijinyakulia pikipiki aina ya SAN MOTO.
Na Hilaly Daudi/GPL