RAPA Roma Mkatoliki amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji lililomkuta yeye pamoja na wenzake watatu usiku wa Jumatano wakiwa katika studio za Tongwe Records zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Roma akielezeawalivyotekwa na kuteswa, kushoto ni mkewe, Mama Ivan
Roma amesema kuwa walikuja watu waliokuwa na silaha za moto, wakawaamuru kuingia kwenye gari na kisha wakafungwa vitambaa usoni na pingu mkononi na kupelekwa eneo ambalo halijulikani.
Wakiwa katika eneo hilo walihojiwa kwa siku tatu huku wakipigwa kabla ya kwenda kutupwa wakiwa wamefungwa katika eneo ambalo kwa haraka hawakujua ni wapi.

Roma akionesha majerah.
Hii ni sehemu ya simulizi aliyoitoa ROMA
“Napenda kuanza kwa kutoa shukrani kwa Mungu, kwenu, kwa wananchi na hasa wasanii wenzangu, pia serikali, nimeona mmesimama imara.
“Jambo lililotokea ni kama case study, kila mmoja amejifunza, leo kwetu, kesho kwa mwandishi na siku nyingine huenda kwa kiongozi wa siasa, hili limetuunganisha wote bila kujali itikadi zetu, tuendelee kushikamana.
“Niseme ukweli tu, mpaka sasa hatuna uhakika na usalama wetu kwa asilimia 100, mahali tulipokuwa si pazuri kabisa.

Waziri Dkt. Mwakyembe akiwasili na ROMA ili kuzungumza na wanahabari.
“Kama alifanyiwa daktari, baadaye akafanyiwa msanii, usishtuke kesho akafanyiwa mwandishi wa habari, au Mbunge.
“Kinachotusikitisha zaidi ni maneno ya baadhi ya watu wanaodai kuwa tumepewa pesa ili tuitengeze hii, siyo sawa.
“Ukweli ni kwamba tukio ni la kweli na tumepigwa sana, hadi sasa hatuko sawa kiafya.

“Siku hiyo, walikuja watu wakiwa na silaha, na wamefunika nyuso zao, wakatuamrisha kuingia ndani ya gari.
“Walitufunga macho na kutupeleka kusikojulikana, walitutesa sana, wametupiga sana.
“Baada ya kupitia katika kipindi cha mateso makali, tuliachiwa usiku, tukaana kutembea bila kujua tuko wapi.
“Siwezi kujua kama tukio hili linahusiana na muziki wangu, maana kuna hadi house boy wetu pia amehusika.

Dkt. Mwakyembe akifafanua
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliyeambatana na ROMA na wenzake ukumbini hapo akaeleza.
“Nilishatoa maagizo, akitokea mtu yeyote mwenye tatizo na msanii, nipewe taarifa kabla msanii huyo hayajakamatwa
“Naomba wasanii tushirikiane kwa pamoja kwenye jambo hili. Kama hatutalikomesha hili, linaweza kuibuka lingine kama hili.
“Siwezi kuzungumzia kauli ya kiongozi aliyesema Roma atapatikana kabla ya Jumapili. Mimi nazungumzia tukio hili, si ya nyuma.
“Upelelezi wa tukio hili hauwezi kuchukua muda mrefu (miezi 6), sababu wahusika wote wapo, nawahakikishia tutapata majibu. Alisema Dkt. Mwakyembe
SIKILIZA ALICHOKIZUNGUMZA ROMA