×

‘Shika Ndinga’ ya EFM, Washindi Wawili wa Pikipiki Wapatikana Tabata

Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia mashindano hayo.

WAKAZI wawili wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Amani Juma na Jeni Haonga, kupitia shindano la Shika Ndinga linaloendeshwa na  Kituo cha Redio cha Efm, lililofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Tabata, walijishindia pikipiki mbili.

Shindano la ‘Shika Ndinga’ linashirikisha wilaya sita za Mkoa wa Dar es Salaam, ambapo muandaaji wa vipindi wa Efm, Dickson Ponela akirudia wito wao kwa wasikilizaji wa kituo hicho cha Efm na kuwataka washiriki kwa wingi kwenye shindano hilo.

Washiriki wakiendelea na mchuano wa Shika Ndinga.

“Tunatoa pikipiki mbili kwa kila wilaya na tumeshatoa pikipiki sita kwa wilaya tatu za Kigamboni, Temeke, Kinondoni na sasa pikipiki mbili zimechukuliwa na wakazi wawili kutoka wilaya ya Ilala na kufikisha idadi ya pikipiki nane ambazo tumeshatoa,” alisema.

Washiriki wakiendelea na mchuano wa Shika Ndinga.

Naye meneja mkuu wa EFM, Dennis Ssebo aliwataka wakazi wa Bagamoyo na Kibaha kukaa mkao wa kula kwani Shika Ndinga inaelekea huko na akasema mwisho wa mashindano watatoa magari mawili aina ya Suzuki Cary.

Pikipiki mbili zinazotolewa kwa kila wilaya, moja huchukuliwa na mwanamke anayeweza kushikilia ndinga (gari) hadi mwisho kwa kuzingatia vigezo vilivyopo. Na pikipiki nyingine inakwenda kwa mwanaume anayeshinda mtihani wa kushikilia ndinga kulingana na masharti yaliyopo.

Washindi wa Shindano la Shika Ndinga, Amani Juma na Jeni Haonga wakiwa katika pikipiki zao walizojishindia.

“Niwaambie kuwa  lengo letu ni kusaidia jamii katika kujikwamua kiuchumi, kwani shindano letu hili linawawezesha wasikilizaji wetu kupata mtaji kupitia zawadi tunazotoa kwani ni zawadi ambazo tunaamini zitawasaidia kuwaingizia kipato,” alisema Ssebo.

Na Hiilaly Daudi/GPL

Leave a Comment