
MSANII wa Bongo Fleva nchini Abednego Damian, ‘Belle9’, amepata pigo baada ya kuondokewa na baba yake mzazi Damian Nyamoga.

Meneja wa Belle9, Jahz Zamba amethibitisha taarifa za hiyo huku akieleza kuwa mzee Damian amefariki dunia kwa kugongwa na bodaboda iliyokuwa kwenye mwendo mkali huko mjini Morogoro ambako alilikuwa akiishi.
Jahz amfunguka kuwa ni pigo kubwa kwa Belle 9 kumpoteza baba yake kwakuwa mara nyingi amekuwa akidai kuwa baba yake ni mwalimu muhimu katika maisha yake. Staa huyo anayetokea Morogoro amelikuwa na mahusiano mazuri na baba yake kama mtu na rafiki yake.
Msiba Upo nyumbani kwa marehemu Morogoro mjini alipokuwa akiishi.