
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amelaumu kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wamesahau misingi ya Muasisi wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja na Azimio la Arusha badala yake wanajifanyia mambo yao wenyewe bila kujali maslahi ya Taifa.
Hayo ameyasema leo wakati akichangia maada Bungeni Mjini Dodoma na kusema;
“Mtatetea vitu vyepesi mnaacha vitu vya msingi, unasema lazima tukimbize mwemge kwa vile upo kwenye Ngao ya Taifa.
” Ngao ina vitu vingi, kama ni hivyo basi tupange root ya kukimbiza na jembe, nyundo na shoka.” “Nembo za Taifa zinaeleweka, inatakiwa tuziheshimu,” alisema Sugu.
Pia Mhe. Sugu amezungumzia suala la Sheria ya Makosa ya Mtandao ‘Cyber Crime’, msikilize hapa akifunguka.