×

Polisi Waua ‘Jambazi’ Akijaribu Kupora Fedha za ATM

 

 JESHI la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema leo  lilifanikiwa kumjeruhi kwa risasi mtu mmoja anayetuhumiwa kuwa jambazi  ambaye baadaye kufariki dunia wakati akijaribu kumpora silaha askari aliyekuwa akisindikiza gari la kampuni ya G4S lililokuwa limebeba fedha Tsh.320,000,000/= zilizokuwa zikisambazwa kwenye ATM za CRDB Bank.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Simon Sirro,  alisema jana maeneo ya Kurasini katika jengo la makao makuu ya Uhamiaji  jambazi huyo ndiko alipotaka kuiba fedha hizo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari.

Alifafanua kuwa katika eneo la tukio kulikuwa na watu wanne waliokuwa kwenye pikipiki mbili aina ya Boxer ambazo hazikusomeka namba na miongoni mwa majambazi hayo ndipo mmoja wao aliruka na kutaka kumpora silaha askari NO. G.8925 PC Adam kwa lengo la kupora fedha na ndipo polisi waliokuwa ndani ya gari la kampuni ya G4S walimpiga risasi za mguuni na kuishiwa nguvu baadaye anadaiwa alifariki wakati akipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Sirro aliendelea kusisitiza kwamba msako mkali bado unaendelea ili kuwakamata watuhumiwa wengine waliokimbia na pikipiki wakati wa tukio hilo.

 

Leave a Comment