×

Gari La Polisi Lanaswa Likibeba Mchanga

Gari la Polisi limenaswa na kamera yetu likisomba mchanga ndani ya mji wa ‘maji kasoro bahari’, Morogoro. Haijajulikana mchanga huo ulikuwa ni wa nani na ulikuwa unakwenda kufanya kazi gani na wapi.

Mwandishi wa mtandao huu alishuhudia watu watatu wakikusanya na kupakia mchanga ndani ya gari hilo la polisi ambalo ni maalum kwa ajili ya Kikosi cha Kutuliza Fujo (FFU) lilikuwa na namba za usajili PT 3725.

(PICHA: MWANDISHI WETU, MOROGORO/GPL)

Leave a Comment