×

Wanafunzi Waadhimisha Siku ya Umuhimu wa Mimea Duniani

Mkurugenzi Mtendaji wa  IITA , Victor Manyong akizungumza na wanahabari.
Ofisa Mawasiliano wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Kilimo cha Kitropiki, Catherine Njuguna akifafanua jambo.
Mtafiti Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Latifa Mrisho (kushoto) akiwapatia wanafunzi wa shule ya msingi waliofika kwenye maabara kujifunza.
… akiwaonesha wanafunzi(hawapo pichani) mti wa muhogo ulio katika maabara hiyo

Taasisi ya kimataifa ya utafiti wa kilimo cha kitropiki (IITA) leo imeadhimisha na wanafunzi Siku ya Umuhimu wa Mimea Duniani kwa kusherehekea kwenye maabara maalum na watoto wa shule ili waweze kujifunza masomo ya kisayansi kwa  bidii.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa  IITA , Victor Manyong amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikijishughulisha  na utafiti wa kilimo ili kuwasaidia wakulima katika mchakato wa kilimo na ndiyo maana siku hii hushirikisha watoto ambao ni vyema wakipata mafunzo tangu awali ili kufikia mafanikio ya kisayansi.

Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa changamoto mbalimbali zimekuwa zikiwakabili wakulima kwa kukosa vitendea kazi vya kisasa pamoja na upungufu wa pembejeo na mbegu.

Maadhimisho ya Siku ya Umuhimu wa Mimea Duniani huadhimishwa Mei 18, kila mwaka.

Na Denis Mtima/GPL

Leave a Comment