×

PICHAZ 13: Mazishi ya Mzee Philemon Ndesamburo

MOSHI: Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82)  ambaye pia ni muasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mzee Philemon Ndesamburo amezikwa leo Jumanne, Juni 6, 2017 nyumbani kwake KDC Moshi huku mazishi yake yakihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo viongozi mbalimbali wa serikali na siasa.

Ndesamburo aliagwa jana katika Uwanja wa Majengo Moshi ambapo leo ibaada ya mazishi ilifanyika katika Kanisa la KKKT Diosisi ya Kaskazini na kuzikwa nyumbani kwake.

Philemoni Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa za mageuzi ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi.

Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi katka siasa na biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake kwa meya wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Wilayani  Karatu mkoani Arusha.

PICHA NA HILLARY DAUDI NA MOHAMMED ZENGWA | GLOBAL TV, MOSHI

VIDEO YA MAZISHI ITAKUWA GLOBAL TV ONLINE HIVI PUDE

Leave a Comment