
NA MWANDISHI WETU | AMANI | SHOWBIZ XTRA
MSANII wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’ amedhamiria kuweka kambi ya muziki nchini Kenya ili kutanua wigo na tayari ameshafanya ngoma kadhaa na wasanii wa nchini humo. Akizungumza na Showbiz Xtra, Matonya aliyeko Kenya kimuziki na kibiashara amesema kuwa hadi sasa ameshafanya ngoma tano na wasanii wa Kenya ambazo hakutaka kuzitaja kwa majina.

“Mapema sana kutaja majina ya hizo nyimbo, lengo langu ni kuweka soko nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla, tayari nimefanya ngoma na msanii Everlast, Kaligraph, Timy na sasa nasubiri kufanya na mkongwe Nyashiski,” alisema Matonya.