×

Mrisho Mpoto Alamba Shavu Ngorongoro

DAR ES SALAAM: Msanii wa muziki wa asili nchini Tanzania, Mrisho Mpoto maarufu kwa jina la ‘Mjomba’ amelamba shavu jingine baada ya kuteuliwa na Mamlaka ya Maliasili na Utalii kuwa msimamizi wa banda la hifadhi ya mbuza ya wanyama ya Ngorongoro.

Mkali huyo wa ngoma ya Sizonje, Mjomba na nyingine, amepewa jukumu na mamlaka hiyo la kuwa msimamizi na mhamasishaji wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Biashara  (Sabasaba) yanayotarajiwa kuanza kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Juni hadi Julai 2017.

Usipitwe, Pata Notifications za Matukio Yote Kutoka GLOBAL TV ONLINE

Leave a Comment