×

Tetesi za Usajili Bongo, Simba na Yanga

Ukimya Wa Simba Wampa Hofu
BEKI wa kulia wa Simba raia wa DR Congo, Janvier Bokungu, amepoteza matumaini ya kuendelea kuitumikia timu hiyo msimu ujao katika michuano ya Ligi Kuu Bara pamoja na ile ya kimataifa kutokana na ukimya wa mabosi wake. Hofu hiyo inatokana na kitendo cha kuchuniwa na uongozi wa timu hiyo tangu alipoondoka nchini na kwenda kwao DR Congo kwa ajili ya mapumziko huku akiahidiwa kuwa ataitwa kwa ajili ya kusaini mkataba mwingine.

“Tangu niondoke Dar es Salaam, sijawasiliana na kiongozi yoyote yule kwa hiyo sijui kama msimu ujao nitakuwa na timu hiyo, waliniambia kuwa wataniita kwa ajili ya kuongeza mkataba lakini naona kimya kimezidi pia nasikia wamesajili wachezaji wawili wenye uwezo wa kucheza nafasi yangu,” alisema Bokungu. Na Sweetbert Lukonge

Ubwa yupo kitaani, mpe anachotaka aichezee timu yako
BEKI wa zamani wa Yanga ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Ndanda FC, Abuu Ubwa, amemaliza mkataba na sasa yupo huru kujiunga na timu yoyote iliyo tayari kumtimizia mahitaji yake.

Beki huyo wa kushoto ambaye aliitumikia Yanga msimu wa 2011/12 kabla ya kwenda Ureno kuichezea Atletico Sport Clube, amesema hawezi kukataa kucheza popote kwa msimu ujao kwani soka ndiyo maisha yake. “Popote nitacheza msimu ujao, ila kwa sasa hakuna timu ambayo imekuja kunifuata baada ya kumaliza mkataba, kikubwa siangalii ukubwa wa timu bali naangalia nitakapoenda nitatimiziwa ninachokihitaji, na si kingine,” alisema Ubwa

Meneja wa Samatta ainyima Yanga mchezaji
WAKATI zoezi la usajili kwa timu mbalimbali za ligi kuu hapa nchini likizidi kushika kasi, meneja wa mshambuliaji wa kimataifa wa KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ameinyima Yanga mchezaji. Mchezaji huyo ni beki wa kati ya Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ambaye inadaiwa kuwa Yanga inapambana viliyo kuhakikisha inamsajili ili aweze kuziba pengo la Mtogo, Vincent Bossou anayedaiwa kutaka kuikacha timu hiyo.

Hata hivyo, habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa, meneja wa mchezaji huyo ambaye ni Jamal Kisongo, hivi karibuni anatarajia kumpeleka Mbonde nchini Serbia kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa. Meneja wa Samatta ainyima Yanga mchezaji

Leave a Comment