Matukio Mbalimbali Viwanja vya Sabasaba Baada ya JPM Kuzindua Maonyesho (+Pichaz)
Global Publishers July 1, 2017 0 Comments
SHARE THIS:
MAMIA ya wananchi wamejitikeza leo katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kushuhudia ufunguzi wa Maonyesho ya Kimataifa ya 41 ya Biashara maarufu kama Maonyesho ya Sabasaba ambayo yamezinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika uzinduzi huo, Rais John Magufuli amewapongeza Watanzania kwa mwamko waliounyesha wakati wa ulipaji wa kodi ya majengo.
Akizungumza leo (Julai 1) wakati akizindua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya Sabasaba, Rais amesema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilipochukua jukumu la kukusanya kodi hiyo imewezesha wananchi kulipa kodi kwa amani.
Msanii Mrisho Mpoto akiwa ni Balozi wa Banda la Mfuko wa Misitu Tanzania
“Walipochukua TRA, sasa waliwathaminishia kodi ambayo wananchi wanaweza kuilipa, ndiyo maana wakajitokeza kwa wingi. Haijapata kutokea wananchi wakataka kulipa kodi kwa kiasi kile, ni kwa sababu ilikuwa nafuu kwao,” amesema
Pia, Rais amewataka TRA kuendelea kukusanya kodi kwa njia ambazo ni rafiki kwa kuwa wananchi hawapendi kodi inayowaumiza bali kodi ambayo ni sahihi kwao.
Banda la Chuo Kikuu UDSM
“Wananchi wanapenda kulipa kodi lakini iwe na manufaa kwako,” amesema
Aidha Rais John Magufuli ameshangazwa na kauli ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo na Biashara nchini Christopher Chiza kuwa na mipango ya kujenga majengo mapya kwa ajili ya wafanyabiashara badala ya viwanda vitakasaidia nchi.
Banda la nyuki
Nyumba ya asili ya kabila la Wagogo
Wananchi wakipatiwa maelekeo kwenye banda la maliasili na misitu.