
Taifa Stars imetinga nusu fainali katika michuano ya Cosafa baada ya kuifunga wenyeji Afrika Kusini bao 1-0.
Shuja wa mechi hiyo ambaye ameibuka nyota wa mchezo huo amekuwa ni Elius Maguri ambaye amefunga bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza.
#FULLTIME #COSAFACup2017 Mwamuzi anamaliza mchezo, Taifa Stars wanapata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Afrika Kusini na kutinga Nusu Fainali pic.twitter.com/6UqWqGhfh6
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 2, 2017
Kipa Aishi Manula mara kadhaa alilazimika kuokoa michomo mikali ya washambuliaji wa Afrika Kusini.
Safu ya ulinzi iliyoongozwa na Erasto Nyoni na Salim Mbonde ilionekana kukaa imara tokea kipindi cha kwanza lakini Muzamiru Yassin na Raphael Alpha wakaonekana kufanya vizuri zaidi katika.
Simon Msuva aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu na kusaidia kuongeza nguvu ya kupandisha presha kwenye lango la Afrika Kusini.
Hongereni @TaifaStars_ watanzania tupo nyuma yenu
— Mbwana Samatta (@samatta77) July 2, 2017