Msanii wa kitambo kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Issa Mussa ‘Cloud 112’ amerejea Bongo kutoka nchini Sweden alikokuwa ameweka makazi yake kwa muda baada ya kutimka Bongo.
Cloud amewasili leo, Julai 3, 2017 ambapo alipokewa na mastaa wenzake sambamba na mashabiki ambapo ujio wake, umekuja sambamba na uzinduzi wa filamu yake mpya aliyorekodi nchini Sweden, iitwayo Usijisahau.
Baada ya kutoka Uwanja wa Ndege, Cloud na timu yake ilielekea moja kwa moja kwenye hoteli ya Lamada ambako hafla fupi ya mapokezi yake sambamba na utambulisho wa filamu hiyo ulifanyika.
Miongoni mwa waliohudhuria mapokezi hayo, ni Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba.