Rais Dkt. John Magufuli amezindua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyamazugo wilayani Sengerema leo ambapo mradi huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2014 kwa gharama ya Sh23 bilioni utawanufaisha zaidi ya wakazi wa wilaya hiyo zaidi ya 13,000 na utahudumia kata 11.
Kata hizo ni Sima, Nyatukala, Ibisabageni, Mwabaruhi, Nyampulukano, Misheni, Tabaruka, Nyampande, Nyamazugu, Nyamazeze na Ibondo.
Mhandisi wa Maji Wilaya ya Sengerema, Nikas Ligombi alisema mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Afrika umekamilika kwa asilima 100 na utakapozinduliwa rasmi tatizo la maji katika mji wa Sengerema litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
“Lita za ujazo 150,000 zitakuwa zinasukumwa kila siku kutoka kwenye chanzo cha maji kwenda kwenye matanki ya kusambaza mitaani,” alisema Ligombi.
Yaliyojili kwenye uzinduzi huo;
#JPMSengerema: Mradi wa maji wa Nyamazugo utafanya upatikanaji wa maji kwa asilimia 100. https://t.co/lNKxiHlF38 pic.twitter.com/gysTja3Qgh
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Mradi wa maji Nyamazugo ni miongoni mwa miradi mikubwa kama ule wa Ruvu Juu Pwani na mingine nchi nzima. @kitilam pic.twitter.com/nBCZrz6qxx
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Mradi wa maji wa Nyamazugo utasaidia hata maeneo mengine ambapo unapita mradi huu. #WillliamNgeleja. –https://t.co/9peghyehXi pic.twitter.com/iwucnuKUGm
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Kada wa #Chadema, aliyewahi kuwa Diwani wa #CCM, Khamis Tabasamu amerudisha kadi kwa @MagufuliJP na kuchukua tena kadi ya CCM pic.twitter.com/7zZnLuAOqb
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#MagufuliMwanza: Mwanamke mjane, Rosemary Linda Saimon mkazi wa Sengerema amemlilia Rais Magufuli akidai kubomolewa nyumba na DAS.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Rais Magufuli anatarajiwa kuzindua mradi wa maji wa Nyamazugo, Sengerema mkoani Mwanza.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge amesema mradi wa maji wa Ng’apa, Lindi uliomchefua Rais Magufuli, umeshakamilika
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Mbali na mradi huu wa Nyamazugo, kuna mradi mkubwa wa maji kwa mkoa huu wa Mwanza unatekelezwa pale Ukerewe. –@MagufuliJP pic.twitter.com/QEHpbbmJmG
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Rais Magufuli amesema alipanga kumfuta kazi Waziri wa Maji, Gerson Lwenge kama angeshindwa kukamilisha mradi wa maji Ng’apa.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Nilikuwa nimepanga kukufukuza Waziri wa Maji endapo mradi wa Ng’apa ungekuwa haujakamilika. – @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: rais Magufuli amewapongeza waziri wa maji Gerson Lwenge na Katibu Mkuu, Kitila Mkumbo kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhusu maji
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Rais @MagufuliJP amewakemea wavuvi haramu wa samaki wanaotumia sumu, awataka waache mara 1,wanahatarisha maisha ya wenzao.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Hizo Ngo’s zijenge shule kwa ajili ya wenye mimba kama wanawapemda sana, mimi sitoruhusu.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Nimekaa Ulaya, hawaruhusu watoto wao kupigwa mimba shuleni, sasa sisi tunakopi kwa nani? –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Tanesco wamekuwa wakinunua umeme kwa senti 500 na kuuza kwa senti 250, hiyo ndo Tanzania, sitaki kusema sana –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Barabara ya ya Kamanga-Sengerema tunaifanyia upembuzi yakinifu, itaanza kujengwa kwa lami kama nilivyoaihidi –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Tunafanya ukaguzi wa pembejeo hewa, watu wameandikwa wamepewa pembejeo kumbe walishakufa. –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Tumeibiwa mno, kwenye madini wametuibia zaidi ya trilioni 300 ambayo ingekuwa bajeti yetu ya miaka 12 –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema:Waliotuibia madini yetu wengine ni viongozi wakubwa wa nchi yetu, mimi nasema ukweli, nafanya hivyo kwa ajili yenu-@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Mimi niliona huu wizi haukuhitaji kusubilia ndio maana ukapelekwa mswada wa dharula bungeni, kuna watu hawataki. –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017
#JPMSengerema: Sijaweza kusafiri kwenda nje ya nchi kwa sababu ukisafiri tu huku wanaiba, sitoki mpaka nisafishe uchafu kabisa –@MagufuliJP.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 4, 2017