×

GlobalSports: Singida United Yamng’oa Winga wa Simba SC

 

KLABU ya Singida United imeipa pigo Klabu ya Simba baada ya kummng’oa winga wake wa kulia, Pastory Athanas na kumsanisha kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu hiyo.

 

Hapo pichani ni Pastory Athans akikabidhiwa jezi na Mratibu Mkuu wa Singida United, Festo Sanga.

 

Pastory Athanas moja ya wachezaji wazuri vijana lakini si chaguo kwa kocha Omog wa Simba, hivyo ameamua kupeleka huduma yake kwa timu ya Singida United Fc.

 

Hili ni pigo jingine kwa Simba baada ya leo watani wao Yanga kumnyakua kiungo wa Ibrahim Ajib na kumsainisha kandarasi ya miaka miwili kukipiga Jangwani.

Endelea kufuatilia taarifa zetu kuhusu tetesi za usajili Bongo na Ulaya.

Leave a Comment